Breaking News

Wednesday, December 14, 2016

Mgeni Rasmi katika kumbukizi ya Marehem Prof. Haroub
Othman wa tatu kulia aliekaa Mh.Ibrahim Mzee Ibrahim
akiwa katika picha ya pamoja na Familia ya Marehem
Prof.Haroub tarehe 03.Diesemba 2016 katika ukumbi wa
ZLSC Kijangwani.

Washiriki mbali mbali waliojitokeza katika Maadhimisho ya
Kumbukizi ya Marehem Prof.Haroub Othman mwanzilishi wa
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar tarehe 03.12.2016

Wa tatu kulia ni Mke wa Marehemu Prof.Haroub Othman Prof.
Saida akiwa na kaka na dada wa Marehemu Prof.Haroub
Katika kumbukizi ya Mume wake iliyofanywa na Kituo
cha Huduma za Sheria Zanzibar tarehe 03.12.2016

Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Mh.Ibrahim Mzee Ibrahim
akizindua Kitabu cha The Econonomy and Freedom of
Communication in Tanzania kilichoandikwa na Mhe.Yose Joseph
Mlyambina tarehe 03.12.2016 katika ukumbi wa ZLSC,Kijangwani.

Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu
Mh.Masauni Yussuf Masauni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi yaliyofanyika katika ukumbi wa ZLSC,Kijangwani tarehe
10.12.2016.

Nd.Abdalla Miraj Othman ndugu wa Marehemu Prof.Haroub
aliesimama akielezea umuhimu wa kuadhimisha siku ya
Sheria Duniani kunakofanywa na Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar kila ifikapo tarehe 10.12.ya kila mwaka.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar Prof.Chris Maina Peter akiwasilisha mada juu
ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na Haki za Binadamu.

Washiriki mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja na
Mgeni Rasmi Mh.Masauni Yussuf Masauni Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maadhimisho ya Siku ya
Haki za Binadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar tarehe 10,Disemba 2016.

No comments:

Post a Comment

Designed By Published. Moonga Stephen