Breaking News

Thursday, February 22, 2018

Read more ...

Wednesday, February 21, 2018

KITABU CHA ZANZIBAR YEAR BOOK OF LAW VOLUME 6 CHAZINDULIWA






Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein,akionesha  kitabu  cha Zanzibar Yearbook of Law Volume 6, 2016 baada ya kukizindua , katika  Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, yaliyofanyika katika Viwanja vya Baraza la Wawakilishi la zamani  Kikwajuni,  tarehe 12 Februari 2018. Kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar  Mhe. Omar Othman Makungu   na kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi Mh. Issa Haji Gavu  


Rais wa Zanzibar na Mwenye Kiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein  amekizindua Kitabu cha Sheria cha mwaka Juzuu ya 6 ( Zanzibar Yearbook of Law (ZYBL), Volume 6) 2016, katika maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika  katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani  Kikwajuni mjini Unguja.

Uwepo wa  ZYBL unatokana na kazi kubwa inayofanywa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kwa kushirikiana na wadau wengine kwa lengo la kutoa uelewa juu ya masuala mbali mbali ya kisheria ya ndani na nje ya nchi. Hivyo ni vyema jamii kukitumia  kitabu hiki.







Read more ...

WASAIDIZI WA WATOTO WAKUMBUSHWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bi. Harusi Miraji Mpatani, akiipitia kwa makini Sheria ya Mtoto Nam. 6  ya mwaka 2011,  katika  mafunzo ya ukumbusho wa Wasaidizi wa Watoto,  yaliyofanyika Kituo cha Huduma za Sheria Kijangwani Zanzibar, tarehe 22 Februari 2018. Katikati  Wakili wa Watoto Wanaokinzana na Sheria Bw. Ahmed  Moh'd  akifuatiwa na Wakili Bi Jamila Masoud 



Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kilifanya mafunzo ya ukumbusho kwa  Wasaidizi wa Watoto kwa  lengo la kuwakumbusha  kazi zao sambamba na kujadili  changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Akifungua  mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bi. Harusi Miraji Mpatani,   aliwataka wasaidizi hao kufanya kazi kwa bidii ili waweze  kufikia malengo yao.

Aidha aliwataka kufanya kazi kwa kushirikiana na Polisi pamoja na Maafisa Dawati ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Nao washiriki wameomba kupatiwa fursa ya kwenda  katika Gereza la watoto ili waweze kujua na kuona mazingira  wanayoishi watoto hao.

Kiongozi wa Wasaidizi wa Watoto  Mkoa wa Kaskazini Unguja Bw. Juma Haji Ali, akichangia katika mafunzo ya ukumbusho wa Wasaidizi wa Watoto yaliyofanyika Kijangwani Zanzibar

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia kwa makini mada ya Watoto wanaokinzana na Sheria pamoja na Haki zao,  iliyowasilishwa na Wakili  Bi. Jamila Masoud  (hayupo pichani),  katika mafunzo ya  ukumbusho wa Wasaidizi wa watoto yaliyofanyika Kijangwani Zanzibar
Read more ...
Designed By Published. Moonga Stephen