Breaking News

Wednesday, February 6, 2019

KITABU CHA SHERIA CHA MWAKA ZANZIBAR TOLEO LA SABA CHAZINDULIWA (ZANZIBAR YEAR BOOK OF LAW VOLUME 7, 2017)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha kitabu cha Sheria  juzuu ya 7, 2017,  (Zanzibar Yearbook of Law  Volume 7, 2017)  baada ya kukizinduwa katika  maadhimisho ya siku ya sherehe yaliyofanyika Pemba. Kushoto ni Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman.

Uwepo wa Kitabu cha Zanzibar yearbook of law umetokana na jitihada kubwa inayofanywa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) kwa kushirikiana na wadau mbali mbali, ambapo mwaka  2011  kilichapishwa kitabu cha kwanza na hadi  sasa kufikia kitabu cha saba.

Lengo la kitabu hiki ni kutoa uelewa mpana juu ya masuala mbali mbali ya kisheria kwa jamii hivyo ni vyema jamii ikakitumia kitabu hiki  kwani kumekukusanya mambo mbali mbali ya msingi na muhimu.
Read more ...

Monday, May 14, 2018

ZLSC YAFANYA MJADALA JUU YA KUMALIZIKA KWA MRADI WA WATOTO WANAOKINZANA NA SHERIA

Wakili wa watoto kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bw. Thabit Abdulla Juma, akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria  kwa Askari Dawati walioshiriki mjadala huo, uliyofanyika  katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani,  tarehe 10 Mei 2018
 Mshiriki akichangia katika mjadala huo uliyofanyika ZLSC Kijangwani, tarehe 10 Mei 2018
 Mshiriki akichangia katika mjadala huo uliyofanyika ZLSC Kijangwani, tarehe 10 Mei 2018
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, Bi Harusi Miraji Mpatani, akifungua mjadala  kuhusu hatma ya Mradi wa Watoto wanaokinzana na Sheria  kwa Mahakimu na Waendesha Mashtaka, uliyofanyika Mazsons Hoteli  Shangani Unguja, tarehe 11Mei 2018
Mahakimu na Waendesha Mashtaka wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Harusi Miraji Mpatani (kati kati) akifungua mjadala  kuhusu hatma ya Mradi wa Watoto wanaokinzana na Sheria,  uliyofanyika Mazsons Hoteli  Shangani Unguja, tarehe 11Mei 2018
Read more ...

Wednesday, May 9, 2018

MKUTANO WA KUJADILI HATMA YA MRADI WA WATOTO WANAOKINZANA NA SHERIA ULIYOFANYIKA TAREHE 5 NA 6 MEI 2018


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, akifafanua jambo  katika mkutano wa kujadili namna ya kuwasaidia watoto baada ya kumalizika kwa mradi wa watoto  wanaokinzana na Sheria. Mkutano huo ulifanyika ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja tarehe  5 Mei 2018. Kushoto ni  Wakili wa watoto Bi. Jamila Masoud Khamis akifuatiwa na Wakili Ahmed Moh'd Abdurrahman

Kituo  cha Huduma za Sheria Zanzibar kilifanya mkutano wa kujadili namna ya kuwasaidia watoto wakati   mradi wa watoto wanaokinzana na sheria ukikaribia  kufikia hatma yake.

Mradi huo ulikuwa ukiendeshwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kwa kushirikiana na UNICEF.

Washiriki wa Mkutano huo walikuwa ni Askari Magereza na Wasaidizi wa watoto ambapo walipendeza watoto waendelee kuwakilishwa mahkamani hata kama mradi utamalizika.

Mradi huo ulianza  2014 na utekelezwaji wake ulianza  tarehe 1 Julai 2015, ukiwa na lengo la kuwawakilisha watoto mahkamani na kuhakikisha wanapata haki zao  kama ilivyobainishwa katika Sheria   ya Mtoto Na 6/2011.

Sheria ya Mtoto Na. 6/2011 katika kifungu cha 43 (1) (e) (iii) kinafafanua haki ya mtoto kuwa na uwakilishi na usaidizi wa kisheria mahkamani.

Awali mradi huu ulikuwa ukiendeshwa kwa Mkoa  wa mjini magharibi pekee  na baadae uliendeshwa   kwa mikoa yote ya Unguja na Pemba ambapo kwa mwaka huu unafikia mwisho.


 Afisa mipango na Wakili  wa watoto kutoka ZLSC Bw. Thabit Abdulla Juma, akitoa maelezo mafupi juu ya Mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria kwa Askari Magereza, katika mkutano uliofanyika ukumbi wa ZLSC Kijangwani, tarehe 5 Mei 2018
Washiriki wakimsikiliza Bw. Ahmed Moh'd Abdurrahman akielezea  changamoto za Mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria, katika mkutano uliofanyika ZLSC Kijangwani, tarehe 5 Mei 2018
 Mshiriki akichangia katika mkutano, uliofanyika ZLSC Kijangwani tarehe 5 Mei 2018
Wasaidizi wa  watoto  wakiwa katika mkutano wa kujadili hatma ya mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria uliofanyika ukumbi wa ZLSC Kijangwani, tarehe 6 Mei 2018
 Mshiriki akichangia katika mkutano huo uliofanyika ZLSC Kijangwani, tarehe 6 Mei 2018


Wasaidizi wa  watoto  wakiwa katika mkutano wa kujadili hatma ya mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria ukiofanyika ukumbi wa ZLSC Kijangwani, tarehe 6 Mei 2018
Read more ...

Thursday, February 22, 2018

Read more ...

Wednesday, February 21, 2018

KITABU CHA ZANZIBAR YEAR BOOK OF LAW VOLUME 6 CHAZINDULIWA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein,akionesha  kitabu  cha Zanzibar Yearbook of Law Volume 6, 2016 baada ya kukizindua , katika  Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, yaliyofanyika katika Viwanja vya Baraza la Wawakilishi la zamani  Kikwajuni,  tarehe 12 Februari 2018. Kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar  Mhe. Omar Othman Makungu   na kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi Mh. Issa Haji Gavu  


Rais wa Zanzibar na Mwenye Kiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein  amekizindua Kitabu cha Sheria cha mwaka Juzuu ya 6 ( Zanzibar Yearbook of Law (ZYBL), Volume 6) 2016, katika maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika  katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani  Kikwajuni mjini Unguja.

Uwepo wa  ZYBL unatokana na kazi kubwa inayofanywa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kwa kushirikiana na wadau wengine kwa lengo la kutoa uelewa juu ya masuala mbali mbali ya kisheria ya ndani na nje ya nchi. Hivyo ni vyema jamii kukitumia  kitabu hiki.Read more ...

WASAIDIZI WA WATOTO WAKUMBUSHWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bi. Harusi Miraji Mpatani, akiipitia kwa makini Sheria ya Mtoto Nam. 6  ya mwaka 2011,  katika  mafunzo ya ukumbusho wa Wasaidizi wa Watoto,  yaliyofanyika Kituo cha Huduma za Sheria Kijangwani Zanzibar, tarehe 22 Februari 2018. Katikati  Wakili wa Watoto Wanaokinzana na Sheria Bw. Ahmed  Moh'd  akifuatiwa na Wakili Bi Jamila Masoud Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kilifanya mafunzo ya ukumbusho kwa  Wasaidizi wa Watoto kwa  lengo la kuwakumbusha  kazi zao sambamba na kujadili  changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Akifungua  mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bi. Harusi Miraji Mpatani,   aliwataka wasaidizi hao kufanya kazi kwa bidii ili waweze  kufikia malengo yao.

Aidha aliwataka kufanya kazi kwa kushirikiana na Polisi pamoja na Maafisa Dawati ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Nao washiriki wameomba kupatiwa fursa ya kwenda  katika Gereza la watoto ili waweze kujua na kuona mazingira  wanayoishi watoto hao.

Kiongozi wa Wasaidizi wa Watoto  Mkoa wa Kaskazini Unguja Bw. Juma Haji Ali, akichangia katika mafunzo ya ukumbusho wa Wasaidizi wa Watoto yaliyofanyika Kijangwani Zanzibar

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia kwa makini mada ya Watoto wanaokinzana na Sheria pamoja na Haki zao,  iliyowasilishwa na Wakili  Bi. Jamila Masoud  (hayupo pichani),  katika mafunzo ya  ukumbusho wa Wasaidizi wa watoto yaliyofanyika Kijangwani Zanzibar
Read more ...

Sunday, December 10, 2017

ZLSC YAADHIMISHA SIKU YA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu  Bw. Mohammed  Khamis akiwasilisha mada ya Dhana ya Haki za Binadamu katika Maadhisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, Kijangwani mjini Unguja.  Kushoto ni Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Bw. Haji Abdalla Haji na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa ZLSC Bi Saida Amour Abdalla

Washiriki wakisiliza mada ya Haki za Binadamu katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja

Mshiriki akichangia mada

Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Mjini Mgharibi Bw. Haji Abdalla Haji  ( aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi  wa ZLSC, Wafanyakazi, na Wadau wengine baada ya  maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika Kijangwani mjini Unguja. Kulia ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu Bw. Mohammed Khamis na  kushoto ni  Mjumbe wa Bodi wa ZLSC Bi. Salma Saadati  

Read more ...
Designed By Published. Moonga Stephen