Tarehe 2 Disemba 2017, Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kiliadhimisha miaka 25 tokea kuanzishwa kwake sambamba na kumbukizi ya muasisi wa Kituo Marehemu Profesa Haroub Othman, iliyofanyika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani, Kikwajuni mjini Unguja.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Haji Ussi (Gavu) ambaye alikipongeza Kituo kwa kuweza kufikisha miaka 25.
Maadhimisho hayo pia yalifuatiwa na uzinduzi wa Kitabu cha Miaka 25 ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar pamoja na kutolewa zawadi kwa waanzilishi wa Kituo na Wajumbe wa Bodi waliotangulia.
|
Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya miaka 25 ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na kumbukizi ya Muasisi wa Kituo Marehemu Prof. Haroub Othman
|
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Haji Ussi (Gavu) akizindua kitabu cha Miaka 25 ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, katika maadhimisho yaliyofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni mjini Unguja, (kati kati) Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, akifuatiwa na Afisa Mipango Bi. Moza Kawambwa Nzole |
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Haji Ussi (Gavu) akionesha kitabu cha Miaka 25 ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, baada ya kukizindua (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi wa Kituo Prof. Chris Maina Peter |
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Haji Ussi (Gavu) akimkabidhi zawadi muanzilishi na aliyekuwa Mjumbe wa Bodi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, Bi. Fatma Maghimbi |
No comments:
Post a Comment