Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bi. Harusi Miraji Mpatani, akiipitia kwa makini Sheria ya Mtoto Nam. 6 ya mwaka 2011, katika mafunzo ya ukumbusho wa Wasaidizi wa Watoto, yaliyofanyika Kituo cha Huduma za Sheria Kijangwani Zanzibar, tarehe 22 Februari 2018. Katikati Wakili wa Watoto Wanaokinzana na Sheria Bw. Ahmed Moh'd akifuatiwa na Wakili Bi Jamila Masoud
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kilifanya mafunzo ya ukumbusho kwa Wasaidizi wa Watoto kwa lengo la kuwakumbusha kazi zao sambamba na kujadili changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bi. Harusi Miraji Mpatani, aliwataka wasaidizi hao kufanya kazi kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao.
Aidha aliwataka kufanya kazi kwa kushirikiana na Polisi pamoja na Maafisa Dawati ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Nao washiriki wameomba kupatiwa fursa ya kwenda katika Gereza la watoto ili waweze kujua na kuona mazingira wanayoishi watoto hao.
Kiongozi wa Wasaidizi wa Watoto Mkoa wa Kaskazini Unguja Bw. Juma Haji Ali, akichangia katika mafunzo ya ukumbusho wa Wasaidizi wa Watoto yaliyofanyika Kijangwani Zanzibar |
No comments:
Post a Comment