Breaking News

Thursday, October 26, 2017

MKUTANO WA MWAKA KWA WADAU WA KITUO (ZLSC)

Kaimu Mkurugenzi Wa Kituo Cha Huduma Za Sheria Zanziabar
Bi Saida Amour akiwasilisha taarifa ya kazi za Kituo kwa mwaka
2017,katika Mkutano hou.




Mmoja wa washidau wa Kituo Bi Suzani Kunambi akichangia
 mada  baada ya kupokea taarifa ya kazi zilizofanywa na
Kituo kwa mwaka
2017.



Read more ...

Tuesday, October 24, 2017

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR KIMEFANYA MAFUNZO YA WASAIDIZI WA SHERIA KWA JUMUIYA YA ZAWOPA(Zanzibar Women Paralegal)


Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kimeandaa  mafunzo ya siku mbili kwa  Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria Wanawake  (ZAWOPA).  Mada mbali mbali  ziliwasilishwa ambazo ni Ndoa na Talaka, Malezi Bora, Matunzo na Ukaazi wa Mtoto kwa Mujibu wa Sheria ya Mtoto, Dhana ya Ugatuzi, Sheria ya Mahakama ya Ardhi pamoja na Rushwa na Changamoto katika Ardhi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza leo tarehe 24 na kumaliza kesho tarehe 25 Oktoba 2017 kwa lengo la kutoa uelewa juu masuala mbali mbali ya kijamii na kuendelea kuwajengea uwezo Wasaidizi wa Sheria waliokwisha hitimu mafunzo yao.


Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma Zanibar
 Bi. Saida Amour Abdalla akifafanua aina za talaka
                                 


Wasaidizi wa Sheria wakifanya kazi za vikundi 



Msaidizi wa Sheria akiwasilisha  kazi ya kikundi






Read more ...

Monday, October 23, 2017

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR KILIFANYA MKUTANO WA KUANDAA MPANGO KAZI

Picha ya pamoja kati ya wajumbe wa bodi, wafanyakazi, washauri na wadau wengine wa ZLSC  katika kuandaa mpango kazi wa Kituo wa mwaka 2018/2022, uliofanyika  Z-Ocean Hoteli,  Bububu Meli nane kuanzia tarehe 14 hadi 16 Oktoba 2017  

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa kuandaa mpango kazi wa Kituo wakimsikiliza kwa makini mshauri

Read more ...

ZLSC YAFANYA TATHMINI YA MAFUNZO YA UTAYARISHAJI KATIBA NA SHERIA KWA VIJANA WA MABARAZA YA VIJANA YALIYOFANYIKA TAREHE 9 OKTOBA 2017

Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Bw. Mohammed Kh. Mohammed akitoa ufafanuzi juu ya tathmini, katika  mkutano wa tathmini ya mafunzo ya elimu ya uraia kwa Vijana wa Mabaraza ya Vijana uliofanyika, ZLSC Kijangwani tarehe 09 Oktoba 2017

Mshiriki  katika mkutano wa tathmini  akielezea kwa washiriki wenziwe  mafanikio aliyoyapata baada ya mafunzo ya elimu ya uraia aliyopatiwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar 

Read more ...

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR KIMEFANYA KONGAMANO LA KUPINGA ADHABU YA KIFO DUNIANI


Read more ...

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR, KILIFANYA MAFUNZO YA HAKI ZA BINADAMU KWA WADAU TAREHE 7 NA 8 OKTOBA 2017 -KIJANGWANI

Washiriki wa mafunzo ya Haki za Binadamu, wakifanya kazi za vikundi  

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Haki za Binadamu  wakifuatilia kwa makini mada ya   dhana ya udhalilishaji iliyowasilishwa na  Afisa Mipango Bi Jamila Masoud ( hayupo pichani)

Read more ...

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE

Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Bi Asya Iddi Hassan ( katikati) akifuatilia igizo kuhusu udhalilishaji ,  lililogizwa na THESODE ,(hawapo pichani),  katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyofanyika ZLSC Kijangwani tarehe 11 Oktoba 2017 wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa ZLSC Bi. Saida Amour Abdalla akifuatiwa na  Mratibu Bi. Jamila Masoud,  wengine ni  Dokta Fatma wa Hospitali ya Mnazi Mmoja  na Bi. Sabra Msellem kutoka DPP 

Wanafunzi wa skuli mbali mbali za Unguja wakisikiliza  mada ya Ukatili wa Kijinsia na Athari za Mimba za Utotoni, iliyowasilishwa  na Dokta Fatma kutoka hospitali ya Mnazi Mmoja 

Read more ...

Friday, October 20, 2017

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR KILIFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KLABU ZA ELIMU YA URAIA KATIKA SKULI ZA MIKOA MITATU YA UNGUJA

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kikiwasili katika moja ya  skuli ilizotembelea ambayo ni skuli ya sekondari Jumbi kwa lengo la kutembelea  klabu ya wanafunzi skulini hapo. 

Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bw. Ali Haji Hassan akiwa na watoto waliopelekwa skuli  na walimu  wa skuli ya Jumbi baada ya watoto hao kukosa  haki ya  elimu bila sababu za msingi na umri ukiwa umesonga ,  Haya ni matunda ya ZLSC baada ya kuwapatia  elimu ya uraia walimu  wa skuli mbali mbali 

Wafanyakazi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bw Mohammed Kh. Mohammed wa (kwanza kushoto) na Bw. Ali Haji Hassan (wa kwanza kulia)   wakiwa na Afisa elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  Bw. Daudi Suhuba  ( alievaa suti ya kijijvu jivu) pamoja na  walimu wa skuli ya Paje,wakizungumzia maendeleo ya klabu  walipofika skulini hapo kutembelea klabu hiyo

Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Ndijani waliojiunga na Klabu ya Elimu ya uraia wakimsikiliza Afisa Mipango  Bw. Ali Haji Hassan ( hayupo pichani) 

Wanafunzi wa  klabu ya skuli ya Paje wakifanya igizo la Udhalilishaji
Wanafunzi wa Skuli ya Kombeni wakiimba wimbo wa  kutokomeza udhalilishaji

Read more ...

ZLSC YAFANYA KONGAMANO LA SIKU YA ADHABU YA KIFO DUNIANI

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, kiliungana na Mataifa mengine duniani kufanya  kongamano la siku ya kupinga Adhabu ya Kifo Duniani ambayo kikawaida hufanyika kila ifikapo tarehe 10.10 kila mwaka.

Kwa mwaka 2017 maadhimisho hayo yalifanyika  kijiji cha Uvivini, kisiwani Tumbatu  kwa Unguja na Ukumbi wa Jeshi la Polisi Chake Chake  kwa Pemba.

Lengo la kongamano hilo ni kukutana na Wadau mbali mbali kwa ajili ya kuelezea hali halisi ya utekelezaji wa hukumu ya kifo na kukusanya maoni.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "UMASIKINI ISIWE SABABU YA KUHUKUMIWA KIFO"



Washiriki wa Kongamano la siku ya kimataifa ya kupinga Adhabu ya Kifo wakiwa safarini kuelekea  kijiji cha Uvivini kisiwani Tumbatu, kwa ajili ya maadhimisho 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar  Prof. Chris Maina Peter ,akitoa ufafanuzi  wa  adhabu ya Kifo kwa  wananchi wa kijiji cha Uvivini kisiwani Tumbatu, katika kongamano la siku ya kimataifa  la kupinga Adhabu ya Kifo Duniani

Mratibu   wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar,  Ofisi ya Pemba Bi. Fatma Khamis Hemed, akiwakaribisha washiriki wa Kongamano la Siku ya kimataifa la kupinga adhabu ya kifo lilifanyika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Chake Chake Pemba   

Washiriki wa Kongamano  wakisiliza kwa makini mada  inayotolewa, katika Kongamano lilifanyika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Chake Chake Pemba

Read more ...

Thursday, October 5, 2017

MAFUNZO YA HAKI ZA BINADAMU KWA WATU WALIOATHIRIKA NA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA YALIYOFANYIKA TAREHE 05 OKTOBA 2017

Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, Bw. Thabit Abdulla Juma akitoa mada ya Haki za Binadamu kwa watu walioathirika na utumiaji wa dawa za kulevya, katika mafunzo yaliyofanyika  ZLSC Kijangwani , mjini -Unguja, tarehe 05 Oktoba 2017

Read more ...

ZIARA YA WANAFUNZI WA SKULI YA SEKONDARI KWARARA KWA KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR

Mwanafunzi wa skuli ya Sekondari Kwarara akielezea  mafunzo aliyoyapata baada ya kuja kituoni katika ziara ya kukitembelea Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, kilichopo Kijangwani mjini Unguja,  ziara hiyo ilifanyika tarehe 03 Oktoba 2017

Read more ...
Designed By Published. Moonga Stephen