Breaking News

Thursday, December 22, 2016

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar Prof.Chris Maina Peter mwenye kanzu na kofia
katikati akiwa katika Dua ya kumuombea Muasisi wa Kituo cha
Huduma za Sheria Zanzibar Prof.Haroub Othman katika Makaburi
ya Familia yaliyopo Chuini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Read more ...
Kina mama wajasiriamali kutoka vikundi vya kina mama wa
kisiwa cha Pemba wakipatiwa Mafunzo ya Haki za Binadamu
na umuhimu wa kina mama hao kujiunga pamoja ili kujikomboa
na umasikini,Mafunzo hayo yaliandaliwa na Kituo cha Huduma
za Sheria Zanzibar ofisi ya Pemba.

Read more ...
Mratibu wa Mafunzo ya Wasaidizi wa Sheria wa Kituo cha
Huduma za Sheria Zanzibar ofisi ya Pemba Safia Saleh
Sultan akizungumza na waandishi wa habari nje ya kumbi wa
Makonyo uliopo Wawi Chake Chake Pemba kuwatambulisha
waandishi dhumuni la Kituo kuendesha Mafunzo ya Wasaidizi
wa Sheria 

Read more ...
Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar
Ofisi ya Pemba Khalfan Amour Mohammed akiwasilisha mada
juu ya jinsi ya kuunda ushirika na umuhimu wa kusajili vikundi vya
ushirika katika Mafunzo ya wanaushirika yaliyofanyika ofisi ndogo
ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ofisi ya Pemba.

Read more ...
Wasaidizi wa Sheria kutoka Pemba wakiwa wanapatiwa Mafunzo
ya utambuzi wa Sheria mpya zilizopitishwa na Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar,Mafunzo hayo yalisimamiwa na Kituo
cha Huduma za Sheria Zanzibar ofisi ya Pemba kwa lengo la
kuwawezesha wasaidizi hao kuitoa elimu hiyo kwa wananchi wa
Majimbo ya Uchaguzi ya Pemba

Read more ...
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ofisi ya Pemba kiliwate
mbelea wananchi wa Mkanyageni siku ya tarehe 13 Disemba
2016 kwa lengo la kuwapatia msaada wa kisheria katika Maa
dhimisho ya Siku ya Msaada wa Kisheria inayoadhimishwa kila
ifikapo tarehe 13 Disemba ya kila mwaka.

Read more ...
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar Josefrieda Pereira wa Pili kulia akikabidhi zawadi kwa
Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii wa tatu kulia Wahida Maabadi,
wanaoshuhudia wa mwanzo kulia ni Bi.Saida Mkuu wa Nyumba
ya kulelea watoto yatima Mazizini na wa mwanzo kushoto ni
Bi.Aisha Mkuu wa Nyumba salama Zanzibar.

Read more ...
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar
Harusi M.Mpatani kushoto akimkabidhi Mkurugenzi wa Ustawi
wa Jamii Wahida Maabani sehemu ya msaada wa Kituo baada
ya Kituo kukutana na Wazee wa Sebleni kwa lengo la kula
 nao chakula pamoja na kuwapatia msaada wa vitu mbali
mbali kama sehemu ya Kumbukizi ya Marehem Prof.Haroub
Othman tarehe 02.Disemba 2016

Read more ...

Wednesday, December 14, 2016

Mgeni Rasmi katika kumbukizi ya Marehem Prof. Haroub
Othman wa tatu kulia aliekaa Mh.Ibrahim Mzee Ibrahim
akiwa katika picha ya pamoja na Familia ya Marehem
Prof.Haroub tarehe 03.Diesemba 2016 katika ukumbi wa
ZLSC Kijangwani.

Washiriki mbali mbali waliojitokeza katika Maadhimisho ya
Kumbukizi ya Marehem Prof.Haroub Othman mwanzilishi wa
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar tarehe 03.12.2016

Wa tatu kulia ni Mke wa Marehemu Prof.Haroub Othman Prof.
Saida akiwa na kaka na dada wa Marehemu Prof.Haroub
Katika kumbukizi ya Mume wake iliyofanywa na Kituo
cha Huduma za Sheria Zanzibar tarehe 03.12.2016

Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Mh.Ibrahim Mzee Ibrahim
akizindua Kitabu cha The Econonomy and Freedom of
Communication in Tanzania kilichoandikwa na Mhe.Yose Joseph
Mlyambina tarehe 03.12.2016 katika ukumbi wa ZLSC,Kijangwani.

Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu
Mh.Masauni Yussuf Masauni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi yaliyofanyika katika ukumbi wa ZLSC,Kijangwani tarehe
10.12.2016.

Nd.Abdalla Miraj Othman ndugu wa Marehemu Prof.Haroub
aliesimama akielezea umuhimu wa kuadhimisha siku ya
Sheria Duniani kunakofanywa na Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar kila ifikapo tarehe 10.12.ya kila mwaka.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar Prof.Chris Maina Peter akiwasilisha mada juu
ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na Haki za Binadamu.

Washiriki mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja na
Mgeni Rasmi Mh.Masauni Yussuf Masauni Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maadhimisho ya Siku ya
Haki za Binadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar tarehe 10,Disemba 2016.

Read more ...
Designed By Published. Moonga Stephen