Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, kiliungana na Mataifa mengine duniani kufanya kongamano la siku ya kupinga Adhabu ya Kifo Duniani ambayo kikawaida hufanyika kila ifikapo tarehe 10.10 kila mwaka.
Kwa mwaka 2017 maadhimisho hayo yalifanyika kijiji cha Uvivini, kisiwani Tumbatu kwa Unguja na Ukumbi wa Jeshi la Polisi Chake Chake kwa Pemba.
Lengo la kongamano hilo ni kukutana na Wadau mbali mbali kwa ajili ya kuelezea hali halisi ya utekelezaji wa hukumu ya kifo na kukusanya maoni.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "UMASIKINI ISIWE SABABU YA KUHUKUMIWA KIFO"
|
No comments:
Post a Comment