Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kimeandaa mafunzo ya siku mbili kwa Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria Wanawake (ZAWOPA). Mada mbali mbali ziliwasilishwa ambazo ni Ndoa na Talaka, Malezi Bora, Matunzo na Ukaazi wa Mtoto kwa Mujibu wa Sheria ya Mtoto, Dhana ya Ugatuzi, Sheria ya Mahakama ya Ardhi pamoja na Rushwa na Changamoto katika Ardhi.
Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza leo tarehe 24 na kumaliza kesho tarehe 25 Oktoba 2017 kwa lengo la kutoa uelewa juu masuala mbali mbali ya kijamii na kuendelea kuwajengea uwezo Wasaidizi wa Sheria waliokwisha hitimu mafunzo yao.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma Zanibar Bi. Saida Amour Abdalla akifafanua aina za talaka |
Wasaidizi wa Sheria wakifanya kazi za vikundi
No comments:
Post a Comment