Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, akifafanua jambo katika mkutano wa kujadili namna ya kuwasaidia watoto baada ya kumalizika kwa mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria. Mkutano huo ulifanyika ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja tarehe 5 Mei 2018. Kushoto ni Wakili wa watoto Bi. Jamila Masoud Khamis akifuatiwa na Wakili Ahmed Moh'd Abdurrahman
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kilifanya mkutano wa kujadili namna ya kuwasaidia watoto wakati mradi wa watoto wanaokinzana na sheria ukikaribia kufikia hatma yake.
Mradi huo ulikuwa ukiendeshwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kwa kushirikiana na UNICEF.
Washiriki wa Mkutano huo walikuwa ni Askari Magereza na Wasaidizi wa watoto ambapo walipendeza watoto waendelee kuwakilishwa mahkamani hata kama mradi utamalizika.
Mradi huo ulianza 2014 na utekelezwaji wake ulianza tarehe 1 Julai 2015, ukiwa na lengo la kuwawakilisha watoto mahkamani na kuhakikisha wanapata haki zao kama ilivyobainishwa katika Sheria ya Mtoto Na 6/2011.
Sheria ya Mtoto Na. 6/2011 katika kifungu cha 43 (1) (e) (iii) kinafafanua haki ya mtoto kuwa na uwakilishi na usaidizi wa kisheria mahkamani.
Awali mradi huu ulikuwa ukiendeshwa kwa Mkoa wa mjini magharibi pekee na baadae uliendeshwa kwa mikoa yote ya Unguja na Pemba ambapo kwa mwaka huu unafikia mwisho.
Washiriki wakimsikiliza Bw. Ahmed Moh'd Abdurrahman akielezea changamoto za Mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria, katika mkutano uliofanyika ZLSC Kijangwani, tarehe 5 Mei 2018
Mshiriki akichangia katika mkutano, uliofanyika ZLSC Kijangwani tarehe 5 Mei 2018
Wasaidizi wa watoto wakiwa katika mkutano wa kujadili hatma ya mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria uliofanyika ukumbi wa ZLSC Kijangwani, tarehe 6 Mei 2018
Mshiriki akichangia katika mkutano huo uliofanyika ZLSC Kijangwani, tarehe 6 Mei 2018
Wasaidizi wa watoto wakiwa katika mkutano wa kujadili hatma ya mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria ukiofanyika ukumbi wa ZLSC Kijangwani, tarehe 6 Mei 2018
No comments:
Post a Comment