Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, kimefanya mafunzo kwa wazazi juu ya malezi salama na mashirikiano ya baba, yaliyofanyika katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja.
Mafunzo hayo ya siku tatu yalikuwa na lengo la kuwashirikisha baba katika malezi ya watoto (Male Engagement on Positive Parenting) kutokana na baba wengi kuwaachia jukumu akina mama na kusahau wajibu wao.
Kupitia mafunzo hayo wanaume walipata elimu ya kutosha juu ya namna ya kushirikiana na wanawake katika malezi ili kuhakikisha watoto wanapata malezi bora na salama.
Mafunzo hayo ya siku tatu yalianza tarehe 10 Septemba 2017 na kumalizika tarehe 12 Septemba 2017.
Wazazi wakiwa katika mafunzo ya malezi salama na mashirikiano ya baba, yaliyofanyika katika Ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja, tarehe 12 Septemba 2017
No comments:
Post a Comment