Kituo kwa kushirikiana na Shirika la PILPG, pamoja na Tume ya Haki za Binadamu na UtawalaBora
Tanzania (CHRAGG) na LHRC kinafanya tafiti juu ya vurugu elekezi (Violent Extremism).
Katika kulifika hili Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kilianadaa mkutano maalum kwa kuwahusisha wadau mbali mbali wakiwemo Jeshi la Polisi, Chuo cha Mafunzo, DPP na Mahakama uliofanyika tarehe Juni 21, 2017 katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja.
Lengo kuu la utafiti huu ni kuangalia mtizamo wa juu kuhusiana na vyombo vinavyohusika na utoaji haki kwa upande wa Zanzibar pamoja na kuangalia njia bora ya kukabiliana na tatizo hilo.
Akizungumza katika mkutano huo Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bw. Ali Haji Hassan alisema , Vurugu elekezi ni kitendo cha kutumia nguvu, kutumia vurugu, au kuhamasisha watu wengine kutumia nguvu au vurugu, ili kufikia malengo fulani ama ya kiitikadi, kidini, kisiasa kijamii au hata kiuchumi.
Washiriki katika mkutano wakichangia mada walisema kuwa ili kulitatua tatizo hili ni vyema jamii ikapewa elimu ya kutosha kwa watu wa rika zote.
Waliitaka jamii ishikamane pamoja kama meno ya vitana ili kuondosha tatizo hili na kupata nchi njema yenye maendeleo endelevu.
Afisa Mipango wa ZLSC akiwasilisha mada kwa wadau mbali mbali |
Msaidizi wa Sheria kutoka Muyuni akichangia mada |
No comments:
Post a Comment