|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein,akionesha kitabu cha Zanzibar Yearbook of Law Volume 6, 2016 baada ya kukizindua , katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, yaliyofanyika katika Viwanja vya Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni, tarehe 12 Februari 2018. Kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Issa Haji Gavu
|
Rais wa Zanzibar na Mwenye Kiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amekizindua Kitabu cha Sheria cha mwaka Juzuu ya 6 (
Zanzibar Yearbook of Law (ZYBL), Volume 6) 2016, katika maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni mjini Unguja.
Uwepo wa ZYBL unatokana na kazi kubwa inayofanywa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kwa kushirikiana na wadau wengine kwa lengo la kutoa uelewa juu ya masuala mbali mbali ya kisheria ya ndani na nje ya nchi. Hivyo ni vyema jamii kukitumia kitabu hiki.
great job https://empireict.net/
ReplyDelete