WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR, RIZIKI PEMBE JUMA AKITOA HOTUBA YA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kimataifa kila mwaka ifikapo Terehe 8 Machi, lengo kuu ni kumuendeleza mwanamke kiuchumi, kijamii, na kisiasa ili kumpa fursa ya kuwa na maendeleleo endelevu.
Kwa kuzinagatia hilo Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kwa kushirikiana na Asasi tofauti zisizo za kiserikali ambazo ni ZAFELA, TAMWA, ZGC, SOS, Action Aid na Save New Generation, wamekuwa mstari wa mbele katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani ambapo Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma, na kauli mbiu ya mwaka huu ilikua"Imarisha fursa za ajira kwa kumuezesha mwanamke kiuchumi" .
Siku ya wanawake duniani ilianza mwanzoni mwa mwaka 1900's kwa kupitia wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani kuandamana kwa kupiga vita udhalilishaji na ukandamizwaji uliokuwa ukitokea katika maeneo ya kazi yakiwemo mazingira magumu na hatari,,ukosefu wa huduma za jamii pamoja na unyanyasaji, .
Kuna mikakati mbali mbali inachukuliwa ili kumuinua mwanamke katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii, ikiwemo kuundwa kwa tume mfano TAMWA. Kuwepo kwa dawati la jinsia, wanawake na watoto, pamoja na kumuinua kielimu kwa kuwawekea skuli maalum mfano Benbella Girls Secondary School ili kuwakuza wanawake kifikra kwa lengo la kupata usawa wa kijinsia kati ya mwanamke na mwanamme.
Jumla ya washiriki 50 walihudhuria maadhimisho hayo wakiwemo Wanaharakati wa Wa Haki za Binaadamu na masuala ya Kijinsia yaliyofanyika tarehe 07/03/2017 katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.
Read more ...