Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha kitabu cha Sheria juzuu ya 7, 2017, (Zanzibar Yearbook of Law Volume 7, 2017) baada ya kukizinduwa katika maadhimisho ya siku ya sherehe yaliyofanyika Pemba. Kushoto ni Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman.
Uwepo wa Kitabu cha Zanzibar yearbook of law umetokana na jitihada kubwa inayofanywa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) kwa kushirikiana na wadau mbali mbali, ambapo mwaka 2011 kilichapishwa kitabu cha kwanza na hadi sasa kufikia kitabu cha saba.
Lengo la kitabu hiki ni kutoa uelewa mpana juu ya masuala mbali mbali ya kisheria kwa jamii hivyo ni vyema jamii ikakitumia kitabu hiki kwani kumekukusanya mambo mbali mbali ya msingi na muhimu.